Sunday, November 4, 2012

RAISI KIKWETE AZINDUA BARABARA YA MINJINGU - BABATI - SINGIDA.

Rais J.K Kikwete akiwa samabamba na mwakilishi wa Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Tonia Kandiero, pamoja na viongozi wengine  wakikata Utepe kuzindua Barabara ya Minjingu - Babati - Singida.

Sehemu ya barabara ya Minjingu - Babati - Singida iliyozinduliwa na Rais Kikwete.


Raisi J.K. Kikwete akiwa na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia kwa Nchi za Uganda, Tanzania na Burundi Bw. Phillipe Dongier, wakiweka jiwe la msingi katika moja ya sehemu inayopita Barabara hiyo katika kijiji cha Mguu wa Zuberi wilayani Monduli.


Mkurugenzi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, BUrundi na Uganda Bw. Phillipe Dongier akipanda mti kama ishara ya kumbukumbu na muendelezo wa ujenzi wa barabara hiyo huku akishuhudiwa na Raisi wa Tanzania Bw. Jakaya Mrisho Kikwete.     

Raisi Kikwete akiwa na Mwakilishi wa Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Bi Tonia Kandiero pamoja na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli (kushoto) sambamba na Waziri Wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Merry Nagu, Wakifurahia kuzinduliwa kwa Barabara ya Manjingu - Babati - Singida.
Raisi kikwete akiwa na Mbunge wa viti maalumu (CHADEMA) Mh. Rose Kamili, Baada ya kuzindua Mradi mkubwa wa Maji wa kijiji cha Mwankonko Mkoani Singida.


Raisi Kikwete akisalimiana na Wananchi waliochanganyika na waandishi wa  Habari mkoani Arusha, mara baada ya kuweka jiwe la Msingi kuainisha muendelezo wa ujenzi wa barabara Minjingu -Babati - Singida.

Picha by Michuzijr.blogspot.com





No comments:

Post a Comment