DJ Topspin kutoa burudani Club 327 Usiku wa Mwaka Mpya
Club
327 leo imetangaza kuwa DJ Topspin wa Marekani ndiye atakayekuwa kwenye moja na
mbili kuwapa burudani wote watakaohudhuria Club hiyo katika kusherekea usiku wa
Mwaka Mpya.
DJ
Topspin amekuwa kipenzi cha watanzania wengi, tokea alipokuja kwa mara ya kwanza
mwaka uliopita katika sherehe za kuadhimisha miaka miwili ya Groove Theory hapa
Dar es Salaam.
Mmiliki
wa Club 327, Lawrence Kadri, alisema uwepo wa DJ Topspin siku hiyo ya mwaka
mpya unaifanya Club 327 kuwa sehemu pekee ya wapenda muziki wa jiji la Dar es
Salaam kuja kufurahia.
‘Sisi
Club 327 tunaamini katika kuwapa wateja wetu upekee katika soko, na ndio maana
tumeifanya Club hii kuwa sehemu maalumu kwa wapenda muziki wote’ alisema Kadri.
‘Kama
mnavyojua, msimu huu wa sikukuu sehemu mbalimbali zimekuwa zikiwaandalia wateja
wao vitu mbalimbali, lakini sisi Club 327 tumeandaa burudani kwa watu ambao
watapenda kusherekea siku ya mwaka mpya stejini’ alisisitiza Kadri.
DJ
Topspin anasifika kwa uwezo wake wa kucheza nyimbo za aina mbalimbali ikiwemo
Top 40, Hip-Hop, Old School, Soulful House, Reggae lakini pia umahiri wake wa
kuwapa wasikilizaji vionjo tofauti wawapo stejini.
Huku
mtindo wake ukijulikana zaidi kama “Cognac-Smooth”, DJ Topspin pia atapata
nafasi ya kusalimiana na baadhi ya wageni waalikwa ukumbini hapo watakokuwa
kwenye chumba maalumu cha Hennessy.
Tanzania
ni mojawapo ya sehemu ambazo DJ Topspin anazikubali kama sehemu za burudani
ambapo anasema, ‘Tanzania ni nchi ambayo ina nafasi kubwa katika moyo wangu,
ikiwa ni nchi pekee niliyoitembelea Afrika ambayo imebadilisha mtazamo wangu
kuhusu bara hili’ alisema Topspin.
Sherehe
za Mwaka Mpya zitaanza rasmi saa tatu kamili usiku tarehe 31, huku DJ Topspin
akitarajiwa kuanza kutoa burudani muda kidogo kabla ya saa sita usiku hadi
asubuhi, kiingilio kikiwa ni shilingi elfu 30,000/-.
No comments:
Post a Comment