Katika kuelekea kuadhimisha siku ya Fistula Duniani, 23/5/2013, Vodacom
kwa kushirikiana na taasisi ys CCBRT wameandaa safari ya kuzunguka nchi nzima inayofahamika
kama ‘Fistula Inatibika’ kutokea Bukoba hadi Dar es Salaam kwenye kilele cha
maadhimisho ya siku hiyo kwenye viwanja vya CCBRT yatakayopokelewa na Rais
Jakaya Kikwete.
Safari hiyo ambayo inahusisha pia kupita kwenye sehemu mbalimbali kuwapa
wananchi ujumbe kuwa Fistula inatibika, itajumuisha pia kukusanya ujumbe kutoka
kwa familia zilizoathirika na Fistula kupeleka kwa Rais hapo tarehe 23 ya mwezi
huu.
Msafara huo utakaochukua jumla ya siku saba, unaongozwa na mwanamuziki
wa kizazi kipya, Hamis Mwinjuma maarufu kama Mwana FA, ambaye atakuwa akiwapa
elimu kuhusiana na Fistula wananchi wa sehemu tofauti tofauti watakaopitiwa na
msafara huo.
|
Meneja Uhusiano wa Mambo ya Nje wa Vodacom Bwana Salim Mwalimu akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Kagera kwenye kampeni ya Fistula Inatibika |
|
MwanaFA akiwaelimisha wananchi wa Geita na kuwahamasisha kutumia fursa hii kujitokeza ili waweze kutibiwa bure |
|
Familia yenye furaha iliyofanikiwa kuushinda ugonjwa wa Fistula kutokana na juhudi za hospitali ya CCBRT pamoja na Vodacom Foundation |
|
Wakazi wa Geita waliojitokeza kwenye kampeni ya Fistula Inatibika |
No comments:
Post a Comment