Monday, July 30, 2012

MWANAMUZIKI DITTO AFIWA NA BABA YAKE MZAZI.

LAMECK DITTO

Mwanamuziki toka jumba la vipaji Tanzania amefiwa na baba yake mzazi usiku wa leo. Ditto akiwa kwenye maeneo ya studio za T.H.T al-maarufu kama "SURROUND SOUND" alipata simu toka kwa ndugu yake ambaye alimpa Taarifa hizo.
Mzazi wake huyo wa kiume anayefahamika kwa jina la Lambeti Tiddo, alifariki masaa machache yaliyopita. Na chanzo cha kifo chake ni ugonjwa wa figo ambao ndio uliokuwa ukimsumbua sana hivi karibuni. Ditto alisema mzee wake huyo alipata nafuu vizuri wiki mbili zilizopita na kurudishwa nyumbani, baada ya kufanyiwa operation iliyokwenda vizuri. Lakini ameshtushwa sana aliposikia mzee wake huyo amezidiwa kiasi kwamba cha kukimbizwa hospitali ya taifa Muhimbili, kwani muda mchache alianza kupata shida ya kupumua vizuri na kuwekewa Oxygen mashine na baada ya muda wa masaa kadhaa kushindwa kabisa kuhema na kufariki dunia.

No comments:

Post a Comment