 |
BARNABA. |
Msanii toka jumba la vipaji T.H.T na mshindi wa tuzo ya Kilimanjaro music awards category ya "TANZANIAN BEST MALE VOCALIST" ELIAS BARNABA, anatarajia kusafiri kwenda nchini Uingereza kushiriki tamasha la AFRICA UNPLUGGED litakalofanyika tarehe 27 mwezi huu katika viwanja vya WEMBELEY ARENA. Tamasha hili linasimama kupinga vita zinazowahusisha watoto "CHILD WAR" na kuhamasisha dunia katika kushirikiana kutatua matatizo mbalimbali yanayolikabili bara la Africa kupitia music, dancing na comedy.
Hata hivyo tamasha hilo litawahusisha wasanii kutoka pembe mbalimbali katika bara la Africa. Atakuwemo Zahara toka south Africa, Fally Ipupa toka Congo, 2face Idibia toka Nigeria, Sarkodie wa Ghana na Femi Kuti toka Nigeria pia toka Africa Mashariki atatoka Jose chamilione wa uganda na Barnaba Tanzania.
No comments:
Post a Comment