Wednesday, July 11, 2012

WASANII WA KIGOMA MFANO WA KUIGWA...

LEKA DUTIGITE KIGOMA.. ni tamasha kubwa linalotarajiwa kufanyika mkoani Kigoma  tarehe 17 ndani ya mwezi huu wa saba na kuwashwa moto na wasanii  wazawa wa kigoma. Mpaka sasa ari waliyonayo wasanii  hao ni ya kubwa mno.. mpaka imekuwa kama ni changamoto kwa wasanii wanaotoka katika mikoa mingine, na kulowea zaidi Dar es Salaam.
Hata hivyo breaking news inaonyesha kuwa karibia nusu ya nyimbo zinazofanya vizuri hivi  sasa katika soko la muziki hapa nchini ni za wasanii wanaotoka katika mkoa wa kigoma. Angalia nyimbo kama "Kichwa kinauma" yake Ali Kiba aliyomshirikisha Jaydee, "Upepo" Recho, "Mawazo" Diamond, "Maneno maneno" Queen Darleen, "Jua ni wewe" Mwasiti akimshirikisha Ally Nipishe, Na nyingine nyingi kutoka kwa wasanii wao kina Chege, Abdu Kiba, Baba Levo, Makomandoo Bongo, Linex, Banana Zorro na wengine wengi.
Jambo lingine la kutia hamasa ni jinsi Mbunge wao wa Kigoma Zitto Kabwe anavyoshirikiana nao katika kila jambo. Naye msimamizi wa ama mratibu wa tamasha hilo Mwasiti Almas naye alifunguka na kusema haya "Kila kitu kwetu kama wasanii wa Kigoma kiko tayari kwa ajili ya tamasha hili, Kilichobaki ni wasanii wenyewe kufika mkoani kwao na kutimiza lengo la Tamasha hili, kwani tamasha hili linasimama kuwatia chachu ama hamasa vijana wa mkoa wa Kigoma mkoani humo". 
Na habari iliyopo hivi karibuni wasanii hao kwa kushirikiana na mbunge wao Zitto Kabwe wanatarajia kufungua Centre ya vijana Kigoma.

Baadhi ya wasanii wa Kigoma leo wakiwa kwenye dinner katika hotel ya Regency.



Mh.Zitto Kabwe akishirikiana na vijana wake katika dinner iliyofanyika katika hotel ya Regency.



Mucky,  Mh.Zitto , Queen Darleen na Mwasiti katika picha.

No comments:

Post a Comment