Wednesday, July 4, 2012

"NI - AMINI" REMIX YA MOTO ILIYOFANYWA NA DITTO...







"Ni-amini" ni wimbo mkali uliowahi kufanywa na Proffessor Jay, Lakini ndani ya  2012 msanii Ditto  ameamua kuurudia wimbo huo kwa staili ya kipekee. Wasanii kama Amini, Angella na Ben Pol.. wote kutoka jumba la vipaji Tanzania (T.H.T) wanaonekana kushirikishwa ndani ya Remix hiyo na kuifanya izidi kunoga. 

Na hapa chini, ni baadhi ya Mistari  mizito na ya moto iliyowahi kuimbwa na Professor Jay enzi hizo, na sasa imerudiwa upya na Ditto....
ANGELLA

"Huhitaji elimu kubwa kutambua
Mapenzi yamekuangukia…
Na hakuna Atakayejiinua
kuyatoa viganjani mwako…
AMINI
Ooh…  Mmmh…   Ooh….

Yapo mazuri yangu, yapo mabaya pia…
Lakini mazuri na mabaya yakikutana…

Yamaanisha kuna binadamu kwenye dunia…"
MARTIN NICHOLSON
BEN POL
Hata hivyo Ditto anasema nyimbo hiyo bado iko jikoni inamaliziwa kupikwa na Martin..  International producer toka UK ambaye anafanyia shughuli zake ndani ya studio za Sorround Sound zilizoko   T.H.T. Na siku atakayokuja kuiachia ngoma hiyo itakuwa ni "BOMB OF THE YEAR"  kwani anaamini kuwa, hata Professor J akija kuisikia lazima awe proud for what Ditto has done!!!

No comments:

Post a Comment