Thursday, August 16, 2012

VAN PERSIE SASA KUCHEZA PAMOJA NA ROONEY MAN U!!!

ROBIN VAN PERSIE

 Mshambuliaji matata toka kwenye kikosi kinachofuliwa na Arsene Wenger (Arsenal)  "ROBIN VAN PERSIE" sasa kuichezea Manchester United. Arsenal ilikubali kumuuza mshambuliaji wake huyo mwenye umri wa miaka 29 na raia wa Uholanzi kwa kitita cha paundi millioni 24.

Kocha wa zamani wa Tottenham, Harry Redknapp na kiungo wa Manchester United Michael Carrick wanaamini kuwa  R.Van Persie atakuwa msaada tosha, na suluhisho la matatizo ya Manchester United na pia atakiongezea nguvu  kikosi hicho kutokana na ufanisi wake wa kazi.

R. Van Persie alifunga mabao yapatayo 44 kwenye mechi 57 alizochezea timu yake na taifa lake yakiwemo mawili dhidi ya Manchester United. Na tayari ameshavionya Vilabu vingine vinavyoshiriki kwenye ligi kuu ya Premier kutarajia upinzani mkali msimu huu.

No comments:

Post a Comment