Monday, December 10, 2012

'KUKUA KWA UCHUMI SABABU YA KUZINDUA CHUPA MPYA ZA HEINEKEN'




Meneja wa Heineken Tanzania, Uche Unigwe, ameelezea sababu za kampuni yake kuzindua chupa mpya za aluminum zenye alama ya nyota za kinywaji hicho kuwa kutokana na kukua kwa uchumi na pia kuongezeka kwa nguvu ya ununuzi katika soko hapa nchini.

"Uchumi unapokua, wateja wanapata nguvu ya kununua, lakini pia uchaguzi wa kile wanachopenda unaongezeka. Uzinduzi wa chupa hizi mpya hasa unataka kuwapa wateja wetu kile wanachopenda, ili kuendana na mitindo yao ya maisha’ alisema Uche.

Unigwe aliongeza kuwa chupa hii mpya ya Heineken ni kiashiria cha bia ya hali ya juu, lakini akasisitiza kuwa ladha ya kinywaji hicho itabaki ile ile inayofurahiwa na zaidi  ya mataifa 170 duniani.


Chupa mpya ya Heineken ilizinduliwwa katika club mpya ya 327, mwishoni mwa wiki hii, ambapo club hiyo pia ilikuwa ikizinduliwa kwa mara ya kwanza.

No comments:

Post a Comment