Uzinduzi
wa club 327 wikiendi hii ulihudhuriwa na wafanyabiashara mbalimbali ambao
walipata fursa ya kuona vyumba maalumu kwa ajili ya kufanyia mazungumzo ya kibiashara
au kubadilishana mawazo vilivyotengenezwa na kinywaji cha Moet na Chandon.
Vyumba
hivyo maalumu vitatu, cha Moet na Chandon, Belvedere na Hennessy vimeunganishwa
na huduma ya DSTV, majokofu yenye vinywaji wakati wote, bafu ya ndani kwa
ndani, pamoja na muziki.
‘Vyumba
hivi ni maalumu kwa kuwakutanisha marafiki wanaofurahia jambo fulani au wateja
wanaojadili biashara mbalimbali’ alisisitiza bwana Kadri.
Hivi
karibuni pia vyumba hivyo vitaunganishwa na mfumo wa simu ambapo wateja
wanaweza kupiga simu kuagiza vinywaji, au kumpigia DJ kuomba mziki wanaoupenda
au kupiga simu nje ya nchi.
‘Sehemu
hakika imeandaliwa maalumu ili kuwapa wateja wafanyabiashara kitu ambacho
kimekuwa kikikosekana sehemu nyingi za burudani’ alisitiza bwana Kadri,
mmilikiwa Bar hiyo.
No comments:
Post a Comment