Sunday, February 10, 2013

Vanessa awakonga mashabiki 'Heineken House'

Andru Mahiga, Vanessa Mdee, Heineken Country Manager-Uche Unigwe, Karabani and Eskardo Bird
Mwanamuziki anayekuja kwa kasi nchini, Vanessa Mdee, ambaye wimbo wake mpya wa Closer umekuwa gumzo hapa nchini na kwingineko, mwishoni mwa wiki hii alipata fursa ya kuwashukuru mashabiki na marafiki katika sherehe iliyoandaliwa na kampuni ya Heineken Tanzania katika ofisi zao hapa Dar es Salaam.

Sherehe hiyo ambayo ilihudhuriwa na mastaa kibao, Vanessa alisimulia historia yake katika muziki na kisha akatoa burudani kwa mashabiki kwa kuimba kibao chake cha Closer, na nyimbo nyingine kadha wa kadha ambazo ameshirikishwa.

Pamoja na burudani kutoka kwa Vanessa, mashabiki pia walipata fursa ya kuburudishwa na kundi zima la B Hitz ambao waliimba wimbo wao mpya wa Press Play, wakifuatiwa na C Pwaa ambaye aliimba wimbo wake wa ‘Mmmh’.

Akimzungumzia Vanessa, Meneja wa Heineken Tanzania, Uche Unigwe alisema kampuni yake inajisikia furaha kushirikiana na Vanessa katika shughuli zake.

‘Hakika tumefurahi kuwa na Vanessa jioni ya leo, kwani amekuwa akituunga mkono katika juhudi zetu za kutangaza kinywaji chetu hapa nchini, na hii ni njia yetu mojawapo kuonyesha shukrani zetu’ alisema Unigwe.

CPWAA
Choice FM presenter-Abby Plaatjes
Vanessa Mdee na shabiki wake
Vanessa akiwaburudisha mashabiki


No comments:

Post a Comment