Mkurugenzi Mkuu mpya wa Zantel, Pratap Ghose akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni |
Dar
es Salaam-April 22,2013: Kampuni ya simu za mikononi ya
Zantel imemteua na kumtangaza, Pratap Ghose, kuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa
Zantel Tanzania.
Kabla ya uteuzi
huu, Pratap ambaye ana miaka 18 ya uzoefu kwenye sekta mbalimbali ikiwemo
mawasiliano alikuwa makamu wa Rais wa Etisalat, Uchumi na ukuzaji wa biashara
kwa kanda ya Afrika.
Pratap anachukua nafasi ya Ali
Bin Jarsh ambaye ameiongoza Zantel kwa miaka miwili na kuipatia mafanikio makubwa.
Bwana Pratap pia
ameshikilia nafasi mbalimbali ikiwemo Afsa fedha mkuu wa kampuni dada ya
Etisalat, India pamoja na kuwa mjumbe wa bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya
Atlantique kanda ya Afrika magharibi.
Pratap pia ana
uzoefu mkubwa wa soko la Tanzania akiwa amefanya kazi kama mshauri wa Zantel na
pia kwa kipndi cha miaka miwili alikuwa Afsa fedha mkuu wa TIGO Tanzania.
Ikizungumzia
uteuzi wake, Zantel Tanzania imesema imefurahishwa na ujio wa bwana Pratap
kwani uzoefu wake kutoka nchi za India, Nigeria pamoja na Mashariki ya Kati
utaipeleka mbali kampuni yao.
Pratap ana shahada
ya juu katika biashara kutoka chuo cha biashara cha Melbourne na pia ni mhasibu
aliyebobea. Akiwa Zantel, Pratap atakuwa na jukumu la kuongeza idadi ya wateja,
pamoja na kusimamia ukuaji wa kampuni na vyanzo tofauti vya mapato.
Pratap Ghose akibadilishana mawazo na Prof. John Nkoma wa TCRA walipokutana hivi karibuni |
No comments:
Post a Comment