Thursday, July 11, 2013

GEMINAH.. VERY INTERESTED GROUP


Have you ever heard about the word Geminah!?? its a new group which contain two of very Talented arstists who are very famous in kanda and nchi nzima ya Tanzania, ambao kila mmoja aliwahi kutamba na vibao vyake kwa wakati wake.
Wanamuziki hao waliojaaliwa sauti za kumfanya shabiki wa muziki aliyekaa chini aweze kusimama, si wengine ni Amini na Barnaba.. ambao wote wawili walisomea muziki katika Chuo cha Muziki na Jumba la Kukuza Vipaji Tanzania THT, sasa wamekuja na ujio mpya wa kuamua kufanya kazi pamoja na kwa mafanikio hivi sasa wameshaachia nyimbo yao mpya inayoanza kupanda kuta za level ya juu katika Playlist za MaDJ mbalimbali katika vituo mbalimbali vya Redio hapa Nchini.

Ili kuisikia ngoma yao mpya click this link.. http://goo.gl/cjADM

Wednesday, July 3, 2013

The Singida Wind East Africa Project Receives Support From President Barack Obama and the White House.



Dar es Salaam, Tanzania, June 30, 2013:  Wind East Africa is proud to share a noteworthy development of our Singida Wind project receiving support from President Barack Obama and the White House in the "Power Africa Initiative" launched June 30th, 2013. 

This comes through our partners Aldwych International which has committed to developing 400 MW of clean, wind power in Kenya and Tanzania – which will represent the first large-scale wind projects in each of these countries, and an associated investment of $1.1 billion. 

This is a much-welcomed development to our project, which already enjoys the support of the Government of Tanzania, Tanesco and the World Bank.

The Shareholders of the Singida Wind East Africa Project are Six Telecoms, Aldwych International and the International Finance Corporation [IFC] the investment arm of the World Bank.


For further information please visit: 

http://m.whitehouse.gov/the-press-office/2013/06/30/fact-sheet-power-africa. 

Friday, May 31, 2013

YAH: MICHANGO YA MAANDALIZI YA MAZISHI YA ALBERT MANGWEHA.


Kamati ya maandalizi ya msiba / mazishi ya msanii ndugu yetu Albert Kenneth Mangweha inapenda kutoa taarifa ya mchakati unaoendelea wa maandalizi ya mazishi, Kamati inahitaji michango yenu kwa ajili ya kufanikisha mazishi pale mwili wa marehemu utakapofika nchini Tanzani,kuanzia kuagwa kwa marehemu shughuli itakayofanyika jijini Dar es Salaam na kusafirishwa mjini Morogoro eneo la Kihonda kwa ajili ya Maziko.
Kusafirisha mwili wa marehemu pekee ni dola za kimarekani elfu sita gharama hizi zimetolewa na Clouds Media Group lakini vilevile kampuni ya Bongo records na Push Mobile kila moja imetoa shilingi milioni tano, EMasters wametoa Tenti 20,viti 1500 na gharama za uwanja wa Leaders pamoja na Mabasi Madogo aina ya coster 5 , Miraji Kikwete ambae yeye amejitolea kuprint tshirt 200 kwa familia na kamati, Samaki samaki wametoa Milioni Moja na Laki tano,skylyte Band wao wametoa gari ambalo litaupokea mwili wa Marehemu na kuusafirisha mpaka Morogoro,

Kwa wale wanaoweza kuchangia kupitia mitandao ya simu tuma kwa kaka wa marehemu Kenneth Mangweha namba zifuatazo:

Tigopesa - +255 717 553905
MPESA - +255 754 967738

Jina la akaunti: Kenneth B Mangweha
Namba ya akaunti: 2012505840
Benki: NMB

Tukitegemea ushirikiano wenu tunatanguliza shukrani za dhati

Monday, May 20, 2013

Msafara wa Fistula Inatibika waelekea Geita



Katika kuelekea kuadhimisha siku ya Fistula Duniani, 23/5/2013, Vodacom kwa kushirikiana na taasisi ys CCBRT wameandaa safari ya kuzunguka nchi nzima inayofahamika kama ‘Fistula Inatibika’ kutokea Bukoba hadi Dar es Salaam kwenye kilele cha maadhimisho ya siku hiyo kwenye viwanja vya CCBRT yatakayopokelewa na Rais Jakaya Kikwete.

Safari hiyo ambayo inahusisha pia kupita kwenye sehemu mbalimbali kuwapa wananchi ujumbe kuwa Fistula inatibika, itajumuisha pia kukusanya ujumbe kutoka kwa familia zilizoathirika na Fistula kupeleka kwa Rais hapo tarehe 23 ya mwezi huu.
Msafara huo utakaochukua jumla ya siku saba, unaongozwa na mwanamuziki wa kizazi kipya, Hamis Mwinjuma maarufu kama Mwana FA, ambaye atakuwa akiwapa elimu kuhusiana na Fistula wananchi wa sehemu tofauti tofauti watakaopitiwa na msafara huo.

Meneja Uhusiano wa Mambo ya Nje wa Vodacom Bwana Salim Mwalimu akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Kagera kwenye kampeni ya Fistula Inatibika

MwanaFA akiwaelimisha wananchi wa Geita na kuwahamasisha kutumia fursa hii kujitokeza ili waweze kutibiwa bure

Familia yenye furaha iliyofanikiwa kuushinda ugonjwa wa Fistula kutokana na juhudi za hospitali ya CCBRT pamoja na Vodacom Foundation

Wakazi wa Geita waliojitokeza kwenye kampeni ya Fistula Inatibika


Monday, May 6, 2013

Zantel yazindua promosheni ya ‘Kwangua na Ushinde’ kwa wateja wa Zanzibar



Mkurugenzi wa Biashara wa Zantel, Zanzibar, Mohamed Mussa akionyesha moja ya zawadi zitakazowaniwa wakati wa uzinduzi wa promosheni ua' Kwangua na Ushinde'. Kulia kwake ni Awaichi Mawalla, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Zantel, na kushoto ni Ibrahim Mussa, Afsa Masoko wa Zantel Zanzibar

Kampuni ya simu za mikononi ya Zantel, leo imezindua promosheni ya ‘Kwangua na Ushinde’ kwa wateja wake wake wa Zanzibar ikiwa ni katika juhudi zake za kuwazawadia wateja wanaotumia mtandao huo.

Promosheni hiyo kubwa ambayo mshindi wake atajinyakulia gari, itawazawadia wateja wengine zawadi za kila siku kama muda wa maongezi wenye thamani ya shilingi milioni  moja, pikipiki aina ya Vespa, komputa ndogo (Huawei Media pads) pamoja na modemu za 3G.

Ili kushiriki katika promosheni hiyo, wateja wapya na wale wa zamani wa Zantel wanapaswa kuweka muda wa maongezi wa kuanzia shilingi elfu moja au zaidi ili kuingia kwenye droo hiyo.

Akizungumzia promosheni hiyo, Mkurugenzi wa Biashara wa Zantel upande wa Zanzibar, Mohamed Mussa, alisema promosheni hiyo inathibitisha nia ya kampuni hiyo katika kuboresha maisha ya wateja wake huku wakiendelea kuwasiliana na ndugu na marafiki zao.

“Tuna furaha kubwa leo kuzindua promosheni hii kwa wateja wetu, ambayo hakika itawapa thamani ya pesa zao kwa kujishindia zawadi mbalimbali’’ alisema Mussa.

Mkurugenzi wa Biashara wa Zantel Zanzibar, Mohamed Mussa akionyesha baadhi ya zawadi zitazogombaniwa wakati wa promosheni ya ‘Kwangua na Ushinde’. Kulia kwake ni Awaichi Mawalla, Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano wa Zantel, Awaichi Mawalla.


Promosheni hii itaendeshwa kwa kipindi cha miezi miwili, kuanzia leo tarehe 6 mwezi wa tano hadi tarehe 6 mwezi wa saba.

Kwa kipindi chote cha promosheni Zantel itatoa jumla ya modemu 60 za 3G, komputa ndogo 12 (Huawei Media pads), pikipiki 6, muda wa maongezi wenye thamani ya shilingi milioni moja pamaoja na gari moja.

“Promosheni hii itaipa kampuni yetu fursa ya kuwasiliana na wateja wetu, huku pia tukiwashukuru kwa kutumia huduma zetu’’ alisisitiza Mussa.

BONUS BALAA

Wakati huo huo kampuni ya Zantel pia imetangaza kuzindua ofa mpya kwa wateja wake wa nchi nzima, iitwayo ‘Bonus Balaa’ ambayo itawapa mara mbili ya muda wa maongezi wakiweka vocha ya kuanzia shilingi elfu moja au zaidi.

Muda huo wa maongezi utawawezesha wateja wa Zantel kupiga mitandao yote.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Zantel, Awaichi Mawalla akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa promosheni mpya ya ‘Kwangua na Ushinde’ pamoja na  ‘Bonus Balaa’. Kulia kwake ni, Mkurugenzi wa biashara wa Zantel, Zanzibar-Mohamed Mussa.