Tuesday, September 18, 2012

NAIBU WAZIRI WA HABARI, VIJANA UTAMADUNI NA MICHEZO MH: AMOS MAKALA ATEMBELEA T.H.T LEO!!!

NAIBU WAZIRI HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO MH. AMOSI MAKALA AKIWA MAENEO YA T.H.T  LEO.

 Naibu Waziri, Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Amos Makala, Leo alitembelea jumba la kukuza vipaji Tanzania  na kujionea na kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa na jumba  hilo.
Makala alipongeza juhudi zinazofanywa na kituo hicho katika kukuza na kuendeleza vipaji hapa nchini, na kusema 'kumekuwa na taarifa nyingi za upotoshaji kuhusu T.H.T, lakini leo nimeonelea nije mwenyewe nione kazi mnazozifanya, na hakika natoa hongera kwa kazi mnayoifanya , kwani inasaidia sana katika kukuza na kupanua wigo wa ajira hapa nchini' alisema makala.

Akimueleza historia fupi ya kituo hicho, Mwanzilishi wa T.H.T Bwana Ruge Mutahaba alisema, 'T.H.T imekuwa na kazi ya kufundisha na kuwaendeleza vijana katika maeneo mbalimbali ya kisanaa. Pamoja na hayo, tunafanya shughuli mbalimbali sana hapa kwetu, ikiwa ni pamoja na kutengeneza filamu na miradi mingine kama kutengeneza historia fupi za watu mbalimbali, matangazo pamoja na kuandaa matamasha mbalimbali'.

Makala pia alitumia ziara hiyo kuzungumza na umoja wa wasanii hapa Tanzania  TANZANIA FLAVA UNIT, ambao waliwakilishwa na mkurugenzi wa umoja huo Hamisi Mwinyijuma almaarufu kama FA, Mhazini wa umoja huo Mwasiti Almasi pamoja na mzungumzaji wake bwana Said Fela, Ambapo walizungumzia swala la studio waliyopewa na Raisi Kikwete mwaka 2009.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Tanzania Fleva Unit, Hamisi Mwinyijuma alisema kikwazo kikubwa cha wao kushindwa kufanya kazi ni kutokana na mvutano uliopo kati yao na chama kingine cha wasanii TUMA. Pamoja na serikali kushindwa kutoa tamko rasmi kuhusu umiliki wa studio hiyo kati yao na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA).
Pia 'Tumefanya mazungumzo mengi kuhusiana na swala hili, lakini kila mara tumeshindwa kufika muafaka.Tunachokuomba mheshimiwa utoe tamko sasa kuhusu umiliki wa studio, lakini pia Serikali imalie mgogoro uliopo kati ya pande hizi mbili, Alisema FA.

Baada ya kusikia pande tofauti, Naibu waziri aliagiza mchakato wa kuanza kuitumia studio uanze chini ya Fleva Unit. kama ilivyoagizwa na Raisi huku serikali ikijipanga kumaliza  mgogoro kati ya Fleva Unity na TUMA.














 








PICHA BY:  RAZACK 4D.

No comments:

Post a Comment