 |
MAKOMANDO BONGO |
Hivi karibuni kundi linaloendeshwa na vijana wadogo kabisa Al-maarufu kama MAKOMANDO BONGO, wanatarajia kuachia video yao mpya kabisa inayokwendaa kwa jina "WAMETOKA MBALI". Ndani ya wimbo huo wamemshirikisha mtoto wa kariakoo Dully Sykes. Video imetumia location ya mikoa tofauti hapa Tanzania, Na kikubwa mno wanasema kaa ujishuhudie jinsi wasanii wengine walivyowapa shavu na kutokelezea kwenye Kideo hicho.
Wimbo umefanywa na studio za Sorround Sound chini ya mkono wa producer Cadrake Touch, huku video ikifanywa na Razack 4D chini ya studio za REDLINE PRODUCTION.
No comments:
Post a Comment