Tanzania House of Talent ama Jumba la vipaji Tanzania a.k.a T.H.T, sasa limekuja na mfumo mpya wa Madarasa.
Zamani jumba hilo lilikuwa likitoa Elimu kwa vijana wenye Vipaji mbalimbali katika tasnia ya muziki kila mwisho wa mwaka kuanzia mwezi wa 12, Lakini sasa jumba hilo limebadili mfumo huo kwa kutoa mafunzo hayo kila mwezi, pamoja na kupanua wigo wake wa mafunzo kwa kuongeza vitu vingi zaidi wakiwemo walimu pamoja na kuyagawanya madarasa katika secta mbalimbali yakiwemo yale ya wanaoimba, kucheza, na wanaojifunza kupiga vyombo mbalimbali vya muziki.
Fomu za kujiunga na madarasa hayo mapya zinapatikana makao makuu ya ofisi hizo zilizopo leaders.
Picha na michuzi junior.
No comments:
Post a Comment