Friday, January 11, 2013

ABDU KIBA AELEZA KILICHOMPATA OMAN!!!

ABDU KIBA.
Baada ya Kupiga show kali katika Hoteli ya Dreams, Hoteli Maarufu ya watu Wazito iliyoko nchini Oman, Abdu kiba ameibuka na kueleza Yaliyomkumba akiwa nchini humo.
Akinza kwa kuielezea Tour yake hiyo iliyopata kuchukua muda wa wiki Mbili katika Utawala wa Kifalme wa Mheshimiwa Qaboon Bin Said Al Said Of Oman, Abdu Kiba Aliamua kuconfess yale yote aliyokutana nayo akiwa Ndani ya Ardhi ya Mfalme huyo. 
"Mimi ni Mswahili pure kabisa toka Bongo, Nimefika kwenye nchi yenye utawala wa watu tofauti na Utawala wa kwetu niliouzoea, But nakiri sijawahi kuona mapokezi ya namna ile, ya watu kuonyesha Upendo na Kumfurahia mgeni kwa kiasi kile Il-hali yule mtu si wa pale".

Abdu, akifurahia na kuwashukuru wale wote waliomsaidia kufanikisha Ziara yake hiyo, huku akizidi kueleza mwenyewe kwa kusema vitu vilivyomtia hamasa akiwa Oman, ni "Kitu nilichofurahia nikiwa kule ni jinsi wale watu wanavyowaguide wageni wao. Nilipewa ulinzi wa kunisindikiza kokote nilipokwenda, Na hata Kwenye time ya show ilipofika Hype ya Mashabiki ilinivutia sana. Na nafurahi kuona Nyimbo zangu za Kizunguzungu Pamoja na Hatuna Habari nao ni Nyimbo zilizopokelewa Vizuri sana Nchini Oman".
Abdu kiba yuko katika harakati za kushughulikia kazi zake mpya ambazo muda si mrefu ataziweka wazi kwa Wananchi.

No comments:

Post a Comment